Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2007
Na Mwandishi Maalumu    .


ABIRIA 28 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Morogoro kuelekea wilayani Kilosa kukosa mwelekeo na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka huu, saa 9.00 alasiri eneo la Kimamba Mkata Ranchi katika barabara ya Kilosa kwenda Morogoro.

Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya basi lenye namba za usajili T 581 AKL aina ya Scania, mali ya Kampuni ya ALI SAID likiendeshwa na Damas Komba (56), mkazi Mkambarani katika Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Andengenye alisema kati ya abiria hao, tisa walitibiwa na kuruhusiwa huku wengine 19 wakiendelea kulazwa katika hospitalini ambapo kati yao 16 walilazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro na wengine watatu kulazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kilosa.

Aliwataja majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa kuwa ni Erick Upanda (36) mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, Mwichande Abdallah (35) mkazi wa Mlandizi, Pwani, Osianga Maumbi (70) mkazi wa Parakuyo Mkata Ranchi Kilosa, Ramadhan Mbuzi (50) mfanyabiashara na Mkazi wa Mji Mpya, Manispaa ya Morogoro, Salum Msangule (42) mkazi wa Ludewa Kilosa.

Wengine ni George Kihando (32) mkazi wa Sinza, Jamila Ibrahim (42) mkazi wa Zombo Kilosa, Sikuza Issa (8) ambaye mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Kigamboni mkoani Dar es Salamu, Amani Mohamed (7) mkazi wa Zombo Kilosa, Nuru Limboka (19) mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam, Samira Mohamed (18) mkazi wa Kilosa, Zaina Athumani (57) mkazi wa Msewe Dar es Salaam.

Wengine ni Konina Rambaya (30) mkazi wa Parakuyo Kilosa, Basiliano Severin (38) mkazi wa Kimamba Kilosa, Halima Ramadhani (26) mkazi wa Kilosa, Nuru Shabani (44) mkazi wa Behewa Kilosa.

Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa ni Kimei Edward (27) mkazi wa Ilonga, Rahabu Josia (56) mkazi wa Magomeni Kilosa na Fahamia Amiry (26) mkazi wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema kuwa hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.



.


..

.
.
.
. .
..
.















..
.

.
.
. . 

.

Leo::
Basi lapinduka na kujeruhi abiria 28
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2007