Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumatano, 25 Agosti 2010) wakati alipokutana na baadhi ya Watanzania waishio Burundi nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi eneo la Kiriri, jijini Bujumbura.

Waziri Mkuu alisema ametembelea nchi kadhaa lakini kila anapofika ubalozini anakuta wanatumia majengo ya kukodi. “Ifike mahali sasa tuseme basi kwa sababu inauma kutoa dola za Marekani 3,000 au 3,500 kila mwezi kumlipa mtu wakati ukiwekeza kwa miaka mitatu unaweza kukamilisha jengo lako…” alisisitiza.

“Tukiweza kujenga ofisi na nyumba zetu tutatoa taswira njema kwamba nasi pia tuna uwezo… nitaendelea kusisistiza jambo hili kwa sababu tunaweza, ni suala la uamuzi tu,” alisema.

Aliwataka mabalozi wa nchi husika wasikate tamaa kuendelea kukumbushia suala hilo hadi Serikali itakapoachana na nyumba za kupanga.

Akizungumza na Watanzania waishio Burundi, Waziri Mkuu aliwaomba waendelee kuishi kwa upendo na mshikamano ili wawe kioo kwa wenyeji wa nchi hiyo na waendeleze sifa nzuri ya Tanzania ya amani na utulivu ambayo imejijengea kwa nchi jirani zinazoizunguka.

Mapema, Balozi wa Tanzania nchini humo Dk. Nzagi alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna Watanzania zaidi ya 3,000 ambao wameishi kwa muda mrefu wakifanya kazi katika mashirika ya kimataifa na wengine ni wafanya biashara.

Waziri Mkuu Pinda yuko jijini Bujumbura akimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule Pierre Nkurunziza (47) kuongoza nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Sherehe hizo zinafanyika leo (Alhamisi, Agosti 26, 2010) kwenye Bunge la nchi hiyo, eneo la Kigobe, jijini Bujumbura.

Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kurejea nchini leo jioni, mara baada ya sherehe hizo kumalizika.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009