Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
RAIS jakaya mrisho kikwete amekiagiza kitengo cha maafa cha ofisi ya waziri mkuu kupeleka magodoro,mashuka na mablangeti kwa wahanga wa mafuriko wilayani kilosa haraka iwezekanavyo.

Akizungumza katika ziara yake ya siku moja wilayani Kilosa jana,rais Kikwete alimtaka afisa mratibu wa kitengo cha maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu bw. Harrison Chinyuka kuhakikisha msaada huo wa magodoro na mablangeti unawafikia wahanga haraka iwezekanavyo.

Amesema haiwezekani ikiwa imetimu miezi miwili sasa toka mafuriko yawakumbe takriban wakazi 26,000 wa wilaya ya kilosa,baadhi yao wawe hawajapatiwa mahitaji hayo muhimu na kuwasababishia adha ikiwemo ya kulala chini.

Amemtaka afisa mratibu huyo wa kitengo cha maafa kuacha kufikiria kusubiri misaada ya magodoro na mahitaji mengine kutoka kwa wahisani wakiwemo UNICEF kwa kuwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inao uwezo wa kununua magodoro na mablangeti yanayoweza kuwatoshereza wahanga wote waliopo makambini.

Akijibu maswali ya rais Kikwete afisa mratibu huyo amesema tayari kitengo cha maafa kimeshapeleka bajeti nzima hazina kwa ajili ya kuidhinishiwa fedha za kununulia mahitaji yote ya lazima na ya muda mfupi.

Rais Kikwete amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro na amerejea jijini Dar e salam kuendelea na shughuli zingine za kitaifa.





























.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009
Na Nickson Mkilanya,Kilosa