Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
Kituo hiki cha Star Tv kimefanikiwa kuchukua nafasi hiyo ambayo pia ilikuwa ikiwaniwa na vituo vya Tbc one na Itv hivyo kuishinda tenda hiyo kutokana na umahiri na ubora wake wa kurusha matangazo ya mpira mara kwa mara.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la soka nchini TFF Afisa habari wa TFF Florian Kaijage amesema kuwa watanzania hususan mashabiki wa soka nchini watarajie kuiona michuano hiyo kupitia kituo hicho.

Star Tv imekuwa na vifaa vya kisasa zaidi katika kurusha matangazo yake likiwemo gari kubwa la matangazo Sports OB Van digitale lenye uwezo wa kutumia kamera zaidi ya kumi kwa mara moja wakati wa kuchukua tukio uwanjani.

Timu kumi na mbili zinashiriki ligi kuu soka Tanzania bara  timu hizo tayari zimeianza michuano hiyo mikubwa nchini.




.



Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009