Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
SERIKALI  imetakiwa  kutoa  mwongozo  haraka juu ya mamlaka  yenye  uamuzi  wa matumizi ya fedha  za maendeleo ya  Sekondari   za kata ili kuondoa  utata uliopo  hivi sasa.


Wito huo umetolewa na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iramba  wakati wakijadili taarifa ya maendeleo  ya elimu  kwenye kikao cha baraza  kilichofanyika mjini Kiomboi.


Madiwani  hao wamesema baada ya  Sekondari hizo  kurudishwa kwa halmashauri  kwa ajili ya usimamizi, hakuna mwongozo juu ya mamna ya kutumia  ruzuku  inayotolewa na serikali  hali inayotoa mwanya  mkubwa kwa wakuu wa shule hizo  kufanya watakavyo wao.


Kutokana na hali  hiyo  madiwani hao wamesema  kuna  haja kwa  serikali  kuhakikisha  kuwa  inatoa haraka  mwongozo  juu ya  utaratibu wa matumizi ya  fedha  za  Sekondari   hizo.


Wamesema kitendo cha kuendelea  kuchelewa kinaweza kusababisha fedha nyingi  zikaishia kwenye  midomo ya wajanja wachache badala ya  kufanya kazi   iliyokusudiwa.


Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri  ya  wilaya ya Iramba bw Fortunatus Fwema  amewataka  madiwani kuwa na subira  kwa madai kuwa  tayari kuna maelekezo maalum yaliyoanza  kutolewa  na serikali juu ya namna ya uendeshaji wa shule  za Sekondari za kata.


Shule  za  Sekondari  za kata awali zilikuwa zinasimamiwa moja kwa moja na wizara ya elimu kabla ya  kukabidhiwa kwa halmashauri na kuteuliwa kwa maafisa elimu  kwa ajili ya shughuli  hiyo.









.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009
Na  Emmanuel Michael , Singida