Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
Aidha, amesema kilimo cha Nyanya kinatoa ajira kwa zaidi ya kaya 35,000 Mkoani Iringa, wengi wao wakiwa vijana.
 
Akizungumza leo (Septemba 2) katika warsha ya kuzindua na kuandaa mpamgo wa uwekezaji katika Mradi wa kuimarisha minyororo ya thamani kwa mazao ya Alizeti na Nyanya, Mpaka  amesema kulingana na taarifa za maendeleo ya kilimo Mkoani Iringa na Shirika la Kilimo Duniani (FAO), zaidi ya asilimia 70 ya Nyanya zinazolishwa nchini Tanzania, huzalishwa Mkoani Iringa.
 
Alisema Soko la Nyanya za Iringa halipo tu ndani ya Tanzania bali lipo pia katika nchi zingine za Afrika kama Kenya, Comoro na  Congo DRC.
 
Hata hivyo, alisema changamoto kubwa ni viwanda vya kusindika Nyanya hiyo ili kuiongezea thamani na hivyo wakulima kunufaika kwani alisema ukiachilia mbali viwanda vilivyopo Mkoani Arusha, Mkoani Iringa kuna viwanda viwili tu vikubwa ambavyo husindika tani 15 kwa siku.
 
Kwa upande wa Alizeti, alisema takwimu za kitaifa za uzalishaji wa mbegu za Alizeti zinaonyesha kuwa Mkoa wa Iringa unazalisha zaidi ya Tani 18,000 kwa mwaka.
 
Kama ilivyo kwenye zao la Nyanya, upande wa viwanda vya kukamua mafuta ya Alizeti pia ni vichache Mkoani Iringa ambapo baadhi ya mbegu za Aliseti zinazozalishwa Mkoani Iringa, hukamuliwa Mkoani Mbeya.
 
Mradi huo ambao unajulikana kama Muunganiko wa Ujasiliamali Vijijini (MUVI) unatekelezwa na makampuni ya Business Care Service (BCS) na Centre for Sustainable Development Initiatives (CSDI) na kusimamia na Wizara ya wiwanda na Biashara kupitia Shirika la viwanda vidogo (SIDO).
 
Kwa mujibu wa Mshauri Mwelekezi Kiongozi wa Timu itakayotekeleza Mradi huo wa MUVI,Hebron Mwakalinga,Mradi huo unaleta mbinu mpya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo vijijini kwa kutumia taratibu iitwayo mnyororo wa thamani (Value Chain) ambapo utaratibu huo unaangalia zao au mazao katika mtiririko mzima kuanzia uzalishaji mashambani, uvunaji, usabazaji pamoja na usafirishaji  hadi masoko.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009