Siku moja baada ya kutokea mauaji ya kutisha ya mkazi mmoja wa mtaa wa misheni Bwana Mapande Mwinamila(38) yanayodaiwa kuongozwa na Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwanza Had Yusuph Kabaju,kamanda wa polisi Mkoa wa mwanza Simon Sirro Ameliagiza jeshi la polisi wilayani hapa kumtia mbaroni Sheikhe huyo na kufanya uchunguzi wa kina kufuatilia mauaji hayo ya kinyama.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu jana Kamanda Sirro alisema jeshi la polisi wilayani humo linatakiwa kuwajibika kwa kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua watakaokuwa wamehusika moja kwa moja kwenye tukio la mauaji hayo iwe kwa kutajwa ama kuhisiwa na bila kujali wadhifa alionao mtuhumiwa katika kesi hiyo.
Mnamo agost 31 mwaka huu majira ya saa 2 usiku katika mtaa wa misheni kijiji cha kalangalala baadhi ya waamini wa dhehebu la kiislam wa msikiti wa masjidil jumaa wakiongozwa na shekhe wao walimvamia nyumbani kwake marehemu Mwinamila(38)ambaaye makazi yake yamepakana na msikiti huo umbali wa mita 20 walimpiga kwa makofi,mateke na ngumi huku wakimpigiza kwenye ukuta wa nyumba yake hadi kuzirai hali iliyopelekea kifo chake.
Kwa mjibu wa Dk Ernest Nkwabi aliyefanyia uchunguzi mwili wa marehemu alisema alipasuka fuvu la kichwa upande wa kushoto jirani na sikio hali iliyosababisha damu kuvuja na kuchanganyika katika ubongo na kusababisha kifo chake.
Kwa mjibu wa mtoto wa marehemu aliyeshuhudia tukio hilo na kuwatambua wauaji akiwemo shehe huyo Majige Mapande alidai kuwa watuhumiwa kwenye mauaji hayo walifikia uamuzi huo baada ya kumtuhumu baba yake kutoa lugha zenye mwelekeo wa kukashifu dini ya kiislam wakati akiwa amelewa pombe.
Lugha za kukashifu dini hiyo zilitolewa na marehemu wakati waamini wa dini hiyo walipotoka msikitini na kufika nyumbani kwa marehemu kutuliza ugomvi wake(marehemu)na mdogo wake Godfrey Mwinamila huku wakimsihi kupunguza kelele zilidodaiwa kuathili shughuli za swala zilizokuwa zikiendelea msikitini hapo.
Hata hivyo marehemu hakuelewa mashairi ya waamini hao wa dini ya kiislamambapo marehemu aliwataka kuondoka nyumbani kwake na dini yao ya kishetani kwa kuwa ugomvi uliwahusu wao na si vinginevyo.
Imezidi kuelezwa kuwa kauli hiyo ya marehemu ilionekana kuwakera watuhumiwa na kuamua kumshushia kipigo cha mbwa mwizi kilichopelekea umauti.
Baadhi ya wananchi na waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali ya waliozungumza na RFA wamesikitishwa na mauaji hayo na kuitaka serikali kupitia jeshi la polisi kuwachukulia hatua waliotenda kosda hilo la kinyama bila kujali wadhifa wa mhusika ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Kufuru hiyo imekuja wakati waamini wa dini ya ya kiislam duniani kote wakiwa katika mfungo mtukufu wa mwezi wa ramadhani huku vuguvugu la kudai kuwepo kwa mahakama ya kadhi nchini likiendelea kufuka moshi.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009