Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
Hayo yalisemwa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil katika mkutano wa mwaka wa Maafisa W aandamizi wa Jeshi hilo uliofanyika jijini Dar-es-salaam kwenye ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini jijini Dar es Salaam.


Akizungumzia juu ya umuhimu wa teknolojia hiyo kwa chombo cha kama hiki, Wakil alilitaka Jeshi hilo kutumia fursa hii kuhakikisha kila mmoja anatekeleza wajibu wake kuhusiana na suala hili hususan kwa kusimamia ukusanyaji wa taarifa zilizoainishwa na kwa muda muafaka.


“Tukumbuke wakati wote kwamba kompyuta haziwezi kutupatia taarifa sahihi na kwa wakati muafaka kama sisi hatutakusanya na kuingiza kwenye kompyuta hizo taarifa sahihi na muafaka” Aliongeza Abdulwakil.


Aliongeza kwamba matumizi ya TEKNOHAMA yanahitaji utekelezaji au uendeshaji unaolandana kwa nchi nzima, hivyo uendeshaji huo utawezesha vyombo vyote vya haki na jinai vya ndani na nje ya nchi kushirikiana na jeshi hilo kwa faida ya pande zote mbili.



Aidha alisema Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kadri ya uchumu utakavyokua ili kuongeza ufanisi na utendaji mzuri Jeshini.



“Chombo cha Magereza ni muhimu katika kuzingatia utawala bora kwa ajili ya kusimamia na maadili ili kuepusha vitendo vya fedheha kwa jeshi hilo, pia Serikali haitakuwa na huruma kwa yeyote atakayebainika kuhusika na kashfa za ufisadi na ubadhilifu wa fedha na mali za Serikali,” alisisitiza.

Aliwataka waumishi wa jeshi hilo, kujiepusha na ugonjwa wa Ukimwi kwa kuwa dawa bado haijapatikana.

Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009