Ukweli wa hali hiyo umebainishwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Juma Mwapachu ambaye anasema kuna umuhimu mkubwa kwa wanachama wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kukaa kwa pamoja na kujadili kwa kina mna ya kuinusuru hali hiyo…
Kauli hiyo inaungwa mkono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Stergomena Tax anayesisitiza kuwa reli ni lazima kwa nchi hizi kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi .
Suala la biashara kupitia usafiri wa reli limeonekana kuchukua uzito wa kipekee kwa sasa kiasi kwamba wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Afrika ya Mashariki wameamua kukutana kwa pamoja kujadili kwa kina namna ya kuboresha huduma hiyo .
Kongamano hilo la siku mbili litakalofanyika jijini Dar es salaam litafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jakaya Mrisho Kikwete.
.
Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009