Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
Akitoa maoni yake kwenye mjadala huo, Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Bw. Kofi Annan alisema kuna haja ya kulinda na kuendeleza sera za kilimo pindi viongozi waliokuwa madarakani wanapoondoka au serikali zinapobadilika.

Bw. Annan ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema mbali ya matatizo yanayozikabili nchi nyingi za Afrika  ya uhaba wa teknolojia, uhaba wa maafisa ugani, ukosefu wa miundombinu bora ya kilimo cha umwagiliaji na ukosefu wa masoko, kuna haja ya kuheshimi sera za kilimo zinawekwa na serikali zilizopo madarakani kama kweli wanataka kuongeza tija katika kilimo cha Afrika.

“Kila mara kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi, viongozi wa Afrika wana tabia ya kuanza kila kitu upya na hili linaua juhudi ambazo zilikuwa zimeanzishwa na wengine… lazima tujifunze kulinda mazuri ya wenzetu bila kujali nani kashinda uchaguzi au nani kachukua nchi (anatawala),” alisema huku akishangiliwa kwenye mkutano huo ulioanza jana (Alhamisi, Septemba 2, 2010) katika ukumbi wa AICC jijini Accra, Ghana.

Naye Makamu wa Rais wa Ghana, Bw. John Dramani Mahama alisema uhakika wa masoko kwa mazao ya wakulima ni eneo jingine ambalo halina budi kupewa kipaumbele ili kuwaidia wakulima wa Afrika wabadili maisha yao.

“Kama kila mkulima atalima chakula kwa ajili ya kulisha familia yake na kujua kuwa anatakaiwa kuzalisha kingine kwa ajili ya kuuza huku akiwa na uhakika kwamba kitanunuliwa, ni wazi kuwa uzalishaji utaongezeka na kuinua maisha ya watu wetu,” alisema.

Akichangia katika mjadala huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema pamoja na kuziangalia upya sera za kilimo katika nchi za Afrika, sera hizo zinapaswa zihusishe pia makundi mengine hasa wanawake na vijana na kuwachukulia kuwa nao ni wadau wa kuleta maendeleo.

“Ni lazima nchi za Afrika ziangalie na ziweke mifumo ambayo inatambulika kisheria ya kuhakikisha kuwa kundi kubwa la wanawake linashiriki katika ngazi za maamuzi ili hata viongozi wanapobadilika au serikali zinapoangushwa kusiwe na mwanya na kupindisha au kuvunja sheria na kubadilisha maamuzi ya serikali zilizotangulia,” alisema.

Akigusia kuhusu vijana alisema, wengi wanakimbia mijini kwa sababu ya ugumu wa kazi ya kilimo, lakini kama wakiwezeshwa katika makundi na kutumia zana za kisasa, lazima watapenda kilimo kwa sababu kuna maeneo ambapo watu wameanza kubaini kuwa ardhi ni mali.

Naye Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Kilimo (IFAD), Bw. Kanayo Nwanze alisema mifumo ya uzalishaji na ununuzi katika kilimo inabidi kuimarishwa ili wakulima wanapozalisha kwa wingi bei zisishuke au wao wasiathirike kwa mazao yao kuoza kwa vile wamekosa wanunuzi.

“Kila mara mkulima akizalisha kwa wingi utasikia matatizo lukuki… ama ataahirika kwa bei kushuka ama ataathirika kwa mazao yake kuoza kwa vile yamemjalia hapo kwa kukosa soko. Lazima tuhakikishe tunawasaidia wakulima kuondokana  na hali hii,” alisisitiza.

Mkutano huo unaendelea leo na utamalizika kesho
Ends 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
03.09.2010



Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009