Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa.
JAMII imetakiwa kujenga utamaduni wa kuyasaidia makundi maalumu yenye matatizo mbalimbali katika maeneo yao .


Wito huo  umetolewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini bibi  Lesi Betheli kwenye  hafla ya kukabidhi msaada kwa wafungwa 21 wa kike wanaotumikia kwenye gereza la wilaya ya Singida na wagonjwa wa hospitali ya mkoa.


Msaada  huo  zikiwemo sabuni za kufulia na kuoga,  vinywaji, biskuiti na pipi ulitolewa na  kikundi hicho kama sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


Bibi Betheli amesema  kuwa  pamoja na kuwepo kwa  makundi mengi maalumu wakiwemo watoto yatima, wajane, wazee, walemavu, wenye  virus  vya  UKIMWI na wafungwa  lakini jamii imesahau kabisa  kutoa misaada na kuona kama sio jukumu lao.


Amesema si busara sana kwa wanawake ambao ni watu wenye huruma nyingi na mapenzi makubwa kwa binadamu wenzao,kuishia tu kusherekea maadhimisho  ya siku yao  kwenye mikutano ya hadhara pekee badala ya  kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye mahitaji.


Kutokana  na hali hiyo amesema kuna haja kwa  watanzania husani wanawake kukumbuka na kutekelezaji wajibu huo muhimu  ili kuyafanya makundi hayo  kuhisi kuwa yanatambuliwa, kuheshimiwa na kuthamini  na jamii inayowazunguka katika maeneo yao.


Radio Free Africa, all rights reserved 1995 - 2009
Na  Emmanuel Michael ,  Singida